Yule anayetahadharisha vitabu vya Shaykh Rabiy´ ni mgonjwa wa moyo

Swali: Baadhi wanasema kuwa hawamnasihi mtu kusoma vitabu vya Shaykh Rabiy´ kwa sababu ndani yake mna ukali. Je, haya ni kweli?

Jibu: Vitabu vya Shaykh Rabiy´ ni vitabu vya Sunnah na itikadi ambazo ni sahihi na zinapambana dhidi ya Bid´ah na kuwalingania watu katika mwenendo mzuri na kuzintengeneza imani za watu na mifumo yao. Haya ndio yenye kutambulika juu ya vitabu vya Shaykh Rabiy´. Yule anayetahadharisha vitabu vyake moyoni mwake mna maradhi; ugonjwa wa Bid´ah na mambo ya utata. Kwa hivyo ni lazima kwake ajirudi juu ya kitendo hichi ambacho ndio sababu ya kuadhibiwa – na ulinzi ni wenye kuombwa kwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=268&size=2&ext=.mp3
  • Imechapishwa: 17/01/2021