Yule anayesema kuwa Imaam Ibn Hajar na Imaam an-Nawawiy ni wazushi


Swali: Ipi nasaha yako kwa yule anayemdiy´ Imaam Ibn Hajar na Imaam an-Nawawiy (Rahimahumu Allaah)?

Jibu: Huyu ndiye Mubtadiy´. Ama Imaam Ibn Hajar na Imaam an-Nawawiy ni maimamu wawili watukufu na ni watu wa Hadiyth. Na wana vitabu vikubwa ambavyo wamestafidi kwavyo Waislamu. Na bado Waislamu wanaendelea kustafidi kwavyo. Na ni katika wanachuoni wa Hadiyth. Haijuzu kuwabadiy´ maimamu hawa wawili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/DwU2RGsH2V0
  • Imechapishwa: 10/03/2018