Swali: Vipi kumraddi mwenye kusema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufa na dalili ya hilo ni pindi tunapomsalia…

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko wapi sasa? Yuko wapi ikiwa kama hakufa? Angelikuwa hai angelitembea na sisi, kukaa na sisi, kupigana vita na sisi na kwenda katika Jihaad. Ameenda wapi? Lau angelikuwa hai tungelimuona. Angelifanya kazi na sisi kama jinsi alivyokuwa akifanya kazi na Maswahabah zake. Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuzikwa? Je, aliye hai huzikwa? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizikwa na wanavyozikwa watu wengine wote; Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) walimzika. Jengine ambalo liko wazi zaidi ni Kauli ya Allaah (Ta´ala):

إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

“Hakika wewe ni maiti [utakufa] na wao pia ni maiti. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenu mtakhasimiana.” (39:30-31)

La jumla kuliko hilo ni Kauli Yake (Ta´ala):

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ

“Kila nafsi itaonja mauti.” (03:185)

Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwanaadamu au sio mwanaadamu? Ni mwanaadamu:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ

“Kila nafsi itaonja mauti.”

Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ الْخُلْدَ ۖ أَفَإِن مِّتَّ فَهُمُ الْخَالِدُونَ

“Na Hatukujaalia kwa mtu yeyote [yule] kabla yako [kuwa] ni mwenye kudumu; Je, basi ukifa wao ni wenye kudumu?” (21:34)

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ

“Na Muhammad si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu?” (03:144)

Ni dalili zinazothibitisha kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atakufa au kuuawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015