Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu.”[1]

Sunnah za makhaliyfah waongofu kunamaanishwa yale waliyokubaliana na sio yale ambayo amepwekeka nayo mmoja wao?

Jibu: Ni yale waliyokubaliana na yale ambayo mmoja wao amepwekeka nayo. Yote ni katika Sunnah za makhaliyfah waongofu.

[1] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa katika ”al-Irwaa’” (2455).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3