Swali: Je, katika Uislamu kuna kitu kinachoitwa ”Taswawwuf ya Kiislamu”?

Jibu: Tunasema kinagaubaga kabisa kwamba hakuna kitu katika Uislamu kinachoitwa ”Taswawwuf” au ”Taswawwuf ya Kiislamu”. Kitu hiki kimezuliwa na kupenyezwa ndani kama yalivyo mambo mengi yaliyoingizwa kati ya waislamu. Baadhi ya mambo hayo yanahusiana na hoja tata ambazo wanafikiri kuwa ni dalili na mengine yanahusiana na kufuata matamanio. Taswawwuf ya Kislamu ni kama mfano wa nyimbo za Kiislamu (أناشيد إسلامية ) –  yote hayo hayana msingi katika Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (34)
  • Imechapishwa: 19/12/2020