Swali: Je, Raafidhwah ni makafiri na khaswakhaswa wale wenye kuwalaani Maswahabah?

Jibu: Ikiwa wanawakufurisha Maswahabah, wanawatia kwenye ufuska, wanawaabudu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au wanasema kuwa Qur-aan haikuhifadhiwa na kwamba kumebaki tu theluthi, hii ni kufuru na kuritadi. Mwenye kuwatukana Maswahabah, akawatia kwenye ufuska au akawatukana amemkadhibisha Allaah.  Kwa sababu Allaah amewatakasa na amewafanya kuwa ni waadilifu. Kumkadhibisha Allaah ni kufuru. Kadhalika kuwaabudu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kuritadi. Tunamuomba Allaah usalama na afya. Mfano wake ni kusema kwamba Qur-aan haikuhifadhiwa na kwamba hakukubaki isipokuwa tu theluthi. Huku pia ni kumkadhibisha Allaah. Kwani amesema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho na hakika Sisi ndio tutaolinda.” (15:09)

Haya yote ni matendo ya kufuru.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638