Swali: Ni ipi hukumu ya kuuza kadi za pongezi juu ya yale yanayohusiana  na sikukuu ya wapendanao?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kuwapongeza mayahudi na wakristo wala kushirikiana nao kwenye sikukuu zao. Hivo ndivo alivosema Shaykh-ul-Islaam na kwamba ni kama mfano wa kuwapongeza kwa ajili ya kusujudia sanamu na kuwapongeza kwa ajili ya kunywa pombe. Kitendo hichi ni khatari. Haijuzu kwa mtu akawapongeza, kuuza kadi zao wala kufanya kitu chochote.

Ni lazima kwa mtu kujichunga kushirikiana na mayahudi na wakristo katika sikukuu zao, kuwapongeza, kuwaalika, kuwapa zawadi kwa mnasaba wa sikukuu zao au kukubali zawadi zao kwa mnasaba wa sikukuu zao. Yote haya ni katika madhambi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 06/06/2020