24Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza: “Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?” 25Petro akajibu: “Naam, hulipa.” Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza: “Simoni, wewe unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?” 26Petro akajibu: “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia: “Haya basi, wananchi hawahusiki. 27Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.”

  • Marejeo: Mathayo 17:24
  • Imechapishwa: 02/02/2020