Yesu akitawadha na akiwatawadhisha wafuasi wake katika Biblia

2Wakati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. 3Yesu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, 4hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. 5Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni.

6Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia: “Bwana, je, wewe utaninawisha mimi miguu?” 7Yesu akamjibu: “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.” 8Petro akamwambia: “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.”

Yesu akamjibu: “Kama nisipokunawisha, wewe huna shirika nami.”

9Ndipo Simoni Petro akajibu: “Usininawishe miguu peke yake, Bwana, bali pamoja na mikono na kichwa pia!”

10Yesu akamjibu: “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Yohana 13:2-10
  • Imechapishwa: 17/01/2020