Yesu akimuomba na akidhihirisha unyonge wake kwa Mola wake

39Yesu akatoka akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata. 40Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake: “Ombeni msije mkaangukia majaribuni.” 41Akajitenga nao, kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti na akaomba 42akisema: “Baba! Kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki, lakini si kama mimi nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 43Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu44Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Luka 22:39-44
  • Imechapishwa: 16/01/2020