Swali: Kuna mtu anaswali, anafunga na anatekeleza nguzo zingine zote za Uislamu. Pamoja na yote hayo anaomba wasiokuwa Allaah kwa njia ya kwamba anafanya Tawassul kwa mawalii, anaomba nusuru kwao, anaitakidi kuwa wana uwezo wa kuleta manufaa na kuzuia madhara. Tunaomba utueleze kama watoto wake ambao wanampwekesha Allaah ambao hawamshirikisha na chochote wana haki ya kumrithi na ni ipi hukumu yao?

Jibu: Ambaye anaswali na kufunga na anatekeleza nguzo zingine za Uislamu lakini hata hivyo anaomba uokozi kwa maiti, Malaika na kadhalika ni mshirikina. Akinasihiwa na asikubali na akaendelea kufanya hayo mpaka akafariki, huyo ni mshirikina aliyefanya shirki kubwa inayomtoa katika Uislamu. Hivyo haoshwi, haswaliwi swalah ya jeneza, hazikwi kwenye makaburi ya waislamu, haombewi msamaha, watoto wake, wazazi wake, ndugu zake na jamaa zake waislamu hawamrithi. Watu hawa hawana dini moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/56)
  • Imechapishwa: 24/08/2020