Kimsingi ni kwamba wudhuu´ wa mwanamke ni sawa na wa mwanaume

Swali: Je, imesuniwa kwa mwanamke wakati wa kufuta kichwa akaanza mwanzoni mwa maoteo ya nywele na kwenda mpaka mwishoni kisha akarudi tena mwanzoni mwa maoteo ya kichwa kama anavyofanya mwanaume?

Jibu: Ndio. Kwa kuwa msingi katika hukumu za Kishari´ah ni kwamba yale yaliyothibiti kwa wanaume yamethibiti vilevile kwa wanawake. Na kinyume chake yaliyothibiti kwa wanawake yamethibiti vilevile kwa wanaume. Isipokuwa kwa kupatikana dalili. Sijui dalili inayomukhusisha mwanamke katika hili. Kujengea juu ya hili mwanamke anatakiwa kupangusa kuanzia maoteo ya kichwa na kupeleka mikono mpaka mwishoni mwa kichwa. Hakuathiri kitu ikiwa nywele ni ndefu. Kwa sababu haina maana kwamba mwanamke anatakiwa kupiga kwa nguvu mpaka nywele zilowe au akapandisha mikono mpaka juu ya kichwa. Inatakiwa kufuta kwa utaratibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/151-152)
  • Imechapishwa: 01/07/2017