Da´wah ya Ahl-ul-Bid´ah na wapotevu ni maradhi. Tazama kwa mfano Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun. Ina zaidi ya miaka thamanini. Matunda yake yako wapi? Wametoa wanachuoni wepi ambao ni al-Ikhwaan al-Muslimuun? Wametoa watu wenye shubuha tu. Kila unaposoma kitabu katika vitabu vyao utakuta tu upotofu. Si kwa sababu nyingine isipokuwa ni kwa sababu hawana elimu sahihi ya Kishari´ah na wahawakusoma chini ya wanachuoni.

Tazama Da´wah ya Jamaa´at-ut-Tabliygh ambayo ina makumi ya miaka tokea wakati ilipoanza. Haikusimama juu ya misingi na matokeo yake ikabaki kama mnavoiona. Ni Bid´ah zilizorithiwa. Mtu hawezi kufuatana nao isipokuwa ni lazima akubaliane na sera zao na mfumo wao. Vinginevyo hawamkubalii kufuata nao. Kuna mtu alinitembelea huko Hijaaz ameshakuwa mtu mzima lakini bado yukohai akanieleza kwamba siku moja walijiwa na Jamaa´at-ut-Tabliygh katika zama ambazo kulikuwa hakuna magari. Wakati huo ngamia na punda ndivyo vilikuwa vipando. Wakaingia msikitini kama kawaida yao na wakawalingania watu watoke na wakawahamasisha juu ya kutoka na kwamba yule mwenye kutoka amepigana katika njia ya Allaah na kwamba yule ambaye hakutoka ameacha kupigana katika njia ya Allaah na kwamba yumo khatarini na wakaeleza kwamba dunia hii ni sanamu miongoni mwa masanamu na mfano wa maneno kama hayo. Akawashaji´isha watu ambapo yule mzee akatoka pamoja nao. Tahamaki akaona wanafanya maovu ambapo aliwaona baadhi yao wanavaa hirizi. Akawaeleza kuwa wametoka hali ya kuwa ni walinganizi na kuwalingania wengine na khaswa katika zama hizi na kwenye mashamba. Hivyo akawaambia kwamba wanatakiwa kukita na kuthibitisha ´Aqiydah ya Tawhiyd kwenye mioyo ya watu hao na kupiga vita mambo ya kishirki na kwamba hirizi ni mambo ya kishirki. Kiongozi wao akamwambia kwamba yeye hivi sasa ni mwenye kuongozwa na sio kiongozi. Hivyo wakamwambia asizungumze kitu; ima afuatane nao hali ya kuwa ni mwenye kuamrishwa na pindi atapopewa ruhusa ya kuongea ataongea. Vinginevyo anyamaze kimya. Mwishowe akaachana nao na hakuwezi kunyenyekea juu ya mfumo wao.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (03)
  • Imechapishwa: 19/05/2019