Yaa Siyn kwa maiti


Swali: Ni ipi hukumu ya kumsomea maiti au yule anayetaka kukata roho Suurah “Yaa Siyn”?

Jibu: Yamepokelewa haya, lakini hata hivyo hayakuthibiti. Kumepokelewa:

“Wasomeeni maiti wenu “Yaa Siyn?”[1]

lakini haikuthibiti. Mtu anayetaka kukata roho anatakiwa kutamkishwa Shahaadah. Atapoitamka asiambiwe tena kutamka. Ikiwa baada ya hapo atatamka maneno, akumbushe kwa mara nyingine kutamka Shahaadah.

[1] Ahmad (4/257) na Abu Daawuud (3121).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2017