Ya wajibu na masharti ya swalah hayapo wakati wa kutokuwa na uwezo

Swali: Kuna mwanamke mzee ameumbwa kiasi cha kwamba hawezi hata kutikisika. Anaacha kuswali kwa sababu nepi zake ni najisi. Unamnasihi nini na vipi atatawadha?

Jibu: Muislamu haachi swalah kwa hali yoyote ile. Maadamu yuko na akili hatakiwi kuacha swalah. Aswali vile alivyo. Hatakiwi kuacha swalah kamwe. Hata kama nguo zake ni najisi na hawezi kujibadili. Hata kama hawezi kutawadha na kufanya Tayammum. Aswali kwa vovyote. Hatakiwi kuacha swalah kamwe. Mambo ya wajibu ya swalah na masharti ya swalah yanakatika wakati wa kutokuwa na uwezo. Hata hivyo kuhusu swalah anatakiwa kuswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqu-%2020-08-1435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015