Wudhuu´ wa swalah ya sunnah kuuswalia faradhi

Swali: Kuna mtu alitawadha kwa ajili ya kuswali swalah ya dhuhaa kisha ukafika wakati wa Dhuhr. Je, inajuzu kwake kuswali Dhuhr kwa wudhu´ wa swalah ya Dhuhaa?

Jibu: Ndio. Akitawadha mtu kwa ajili ya kusoma Qur-aan au kuswali swalah ya dhuhaa bado anaendelea kubaki na wudhuu´ wake. Hivyo aswali Dhuhr, ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa mpaka wudhuu´ wake uchenguke. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya kufunguliwa mji wa Makkah aliswali swalah tano kwa wudhuu´ mmoja. Wakati ´Umar alipomuuliza na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Nimefanya jambo ambalo wewe hukufanya.” Akasema: “Ee ´Umar! Nilikusudia kufanya hivo.” Bi maana kwa ajili ya kubainisha kwamba inajuzu. Kwa hivyo mtu akitawadha kwa ajili ya kusoma Qur-aan, kuswali dhuhaa au akatawadha kwa ajili ya kuswali sunnah atakazoweza – hata kama itakuwa wakati usiokuwa wa dhuhaa – basi midhali yuko katika twahara aswali endapo utakuja wakati wa swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 07/03/2018