Wudhuu´ wa mtu aliye na mafuta ya mgando ni sahihi?

Swali: Wudhuu´ wa mtu ni sahihi akiwa na mafuta mikononi mwake?

Jibu: Ndio, wudhuu´ wake ni sahihi kwa sharti mafuta haya yasiwe yanazuia maji kufika kwenye [ngozi]. Ikiwa mafuta haya ya kuganda yanazuia maji kufika, basi ni lazima kuyaondosha kwanza kabla ya kutawadha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/147)
  • Imechapishwa: 30/06/2017