Wudhuu´ wa ambaye amekatwa mguu au mkono


126- Nilimuuliza baba yangu  kuhusu mtu ambaye mkono wake umekatwa hadi kwenye kiwiko. Akajibu:

“Ataosha mkono wake mpaka mahali alipokatwa. Ataugeuza na kupangusa.”

Nilimuuliza baba yangu kuhusu mtu ambaye mguu wake umekatwa. Akajibu:

“Ataosha mpaka pale pahali alipokuaga akitawadha.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/105)
  • Imechapishwa: 23/01/2021