Wudhuu´ umeharibika kabla ya Tasliym ya pili


Swali: Kuna mtu wudhuu´ wake ulichenguka baada ya Tasliym ya kwanza na kabla ya Tasliym ya pili. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Wudhuu´ wake umechenguka kabla ya Tasliym ya pili. Ikiwa umechenguka kabla ya Tasliym swalah yake inaharibika. Hata hivyo swalah yake ni sahihi ikiwa umechenguka baada ya kutoa Tasliym.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (58) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16539
  • Imechapishwa: 23/09/2017