Wudhuu´ kwa ambaye ana mguu bandia

Swali: Kuna mtu ana mguu bandia. Atawadhe vipi?

Jibu: Si wajibu. Anatakiwa kuosha ule mguu mwingine. Kuhusu ule mguu wa bandia uwajibu wake umeanguka midhali mguu wake umekatwa kuanzia kwenye vifundo vya miguu. Wapo wanachuoni waliosema kuwa anatakiwa kuosha kichwa cha muundi ukiwepo. Lakini ikiwa mguu wake ni wa bandia ina maana ya kwamba [uwajibu wake] umeanguka na hauna nafasi. Anachotakiwa ni yeye kutawadha na kuosha viungo vyengine. Ama ule mguu uliokatwa hakuna haja. Ni kama mfano akikatwa kidole chake kimoja [uwajibu wake] unaanguka kwa kule kukatwa kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2018