Swali: Kumfanyia uasi mtawala kunakuwa kwa silaha peke yake au kunaingia vilevile kuwaponda watawala?

Jibu: Yote mawili ni kufanya uasi. Yule ambaye anawachochea watu kwa maneno huyu ni katika wakaaji. Ibaadhiyyah ni katika wakaaji. Wanachochea katika Jihaad lakini wao hawatoki. Wanawachochea watu lakini wao hawatoki. Hawa ni Khawaarij wenye kukaa. Wanaitwa ´wakaaji`. Kuhusu yule anayefanya uasi kwa silaha jambo lake liko wazi ya kwamba ni Khaarijiy. Huyu amefanya uasi kwa silaha. Wote wawili ni Khawaarij. Ni mamoja huyu na yule.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 61
  • Imechapishwa: 30/07/2017