Swali: Je, ni kweli kwamba waislamu na mayahudi wanamwabudu mwabudiwa mmoja?

Jibu: Mayahudi wanamwabudu mungu Mmoja? Mayahudi ni washirikina. Amesema (Ta´ala):

وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ

“Mayahudi wanasema: ‘Uzayr ni mwana wa Allaah” na manaswara wanasema: “al-Masiyh ni mwana wa Allaah”.”[1]

Ni wenye kumshirikisha Allaah. Baada ya kutumilizwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi mayahudi, manaswara na dini nyenginezo zote, ni lazima kwao kuingia katika Uislamu:

فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Basi wale waliomuamini na wakamtukuza na wakamnusuru na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.”[2]

Haitoshi kuamini pasi na kumfuata  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 09:30

[2] 07:157

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 11/05/2021