Imaam Ahmad bin ´Aliy al-Maqriyziy anasema:

“Na kila mwenye kutanguliza kauli isiyokuwa ya Allaah kabla ya kauli ya Allaah, akahukumu kwayo au akahukumiwa kwayo, sio katika wale wanampenda.”[1]

Anayempenda Allaah hutanguliza kauli ya Allaah na ya Mtume Wake kabla ya fulani na fulani. Ikiwa anatanguliza kauli ya Shaykh wake, imamu wake, kipote au kundi lake kabla ya amri ya Allaah, huyu ni muongo anapodai anampenda Allaah (´Azza wa Jalla). Kaacha Shari´ah ya Allaah na kuhukumiwa kwa kanuni za binaadamu. Je, huyu kweli anampenda Allaah (´Azza wa Jall)? Ni muongo. Yaani akahukumiwa kinyume na isiyokuwa Shari´ah ya Allaah. Huyu ni muongo akisema kuwa anampenda Allaah. Na hili si khaswa migogoro mahakamani, kama wanavyofahamu baadhi ya watu. Bali ni katika migogoro yote na tofauti. Mtu atangulize kauli ya Allaah na kauli ya Mtume Wake na wala asitangulize kauli ya yeyote. Katika masuala ya Ijtihaad, ´Aqiydah na katika masuala yote yenye tofauti.

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ

”Jambo lolote lile mlilokhitilafiana kwalo, basi hukumu yake ni kwa Allaah. Huyo ndiye Allaah, Mola wangu, Kwake nategemea na Kwake narejea kutubia.”[2]

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[3]

Sio khaswa mahakamani tu. Hili ni jumla kwa kila tofauti ilioko baina ya watu. Anatanguliza utiifu kwa Allaah na Mtume Wake kabla ya kauli ya fulani na fulani, madhehebu na yasiyokuwa hayo. Hata ikiwa atadai yeye anampenda Allaah nakadhalika. Tunamwambia wewe ni muongo. Hukuhakikisha madai uliosema.

[1] Tajriyd-ut-Tawhiyd, uk 102.

[2] 42:10

[3] 04:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/tg–1431-11-11.mp3 Tarehe: 1431-11-11/2010-10-18
  • Imechapishwa: 09/04/2022