Swali: Tulipokuwa watoto wadogo tulikuwa tukiiba kwenye maduka na hapo ilikuwa miaka thelathini iliyopita na wala hatuwajui wamiliki wa hayo maduka. Hivi sasa Allaah ametuongoza na tumetubia. Je, hatuna dhambi kwa yaliyopita kutokana na neno Lake (Subhaanah):

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ

“Waambie waliokufuru kwamba: wakikoma watasamehewa yale yaliyopita.”[1]?

Jibu: Hapana. Ni lazima kuwarudishia watu haki zao. Kuhusu haki za Allaah ni kweli kwamba Allaah anazisamehe. Lakini haki za watu ni lazima ima mwenye nayo aisamehe au uwarudishie nayo. Lakini ikiwa huwajui basi unachotakiwa ni wewe kutoa swadaqah kiwango kile ulichochukua kwa nia ya kwamba thawabu zake ziwaendee wale uliochukua kutoka kwao.

[1] 08:38

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (74) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-25-01-1439H-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/11/2017