Witr wakati wa Maghrib


Swali: Nikiwa safarini na nikaswali Maghrib na ´Ishaa wakati wa swalah ya Maghrib itafaa kwangu kuswali Witr wakati wa swalah ya Maghrib?

Jibu: Ndio, inafaa kufanya hivo. Ukimaliza kuswali ´Ishaa umeingia wakati wa Witr juu yako. Lakini bora ni kuchelewesha Witr mpaka mwishoni mwa usiku au kabla ya kwenda kulala.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 18/06/2021