Witr wakati wa adhaana ya Fajr


Swali: Inafaa kuswali swalah ya Witr muadhini akiadhini kwa ajili ya swalah ya Fajr?

Jibu: Ikiwa ameshaianza basi aikamilishe. Lakini hapana ikiwa ndio ameianza. Kwa sababu adhaana ya Fajr inafidisha dhana ya juu na haifidishi yakini ya juu. Kwa sababu muadhini anaadhini kwa mujibu wa kalenda. Ama ikiwa ameona kweli kwamba alfajiri imechomoza jangwani basi adhaana yake inafidisha yakini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 14/05/2019