Wito wa kuwasitiza wafungaji kula na kunywa alfajiri

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa wito kupitia kipaza sauti kabla ya adhaana ya fajr kwa ibara ifuatayo:

“Kunyweji maji na harakisheni. Kunyweni maji kabla alfajiri haijaingia.”?

Jibu: Hii ni Bid´ah. Ni Bid´ah kuanzia hivi sasa kabla alfajiri haijaingia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na sisi hivi sasa tunabakiza saa moja kabla ya kuingia magharibi, hakutuwekea katika Shari´ah kusema hivi. Alichosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwazindua Maswahabah wake ni:

“Hakika Bilaal ni mtu anayeadhini usiku. Hivyo basi, asikuzuieni chakula chenu na kinywaji chenu. Kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum. Kwani ni mtu kipofu na haadhini mpaka aambiwe “Kumepambazuka! Kumepambazuka!”

Akiadhini muadhini mambo kwisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni na kunyweni mpaka aadhini… “

Hii sio adhaana. Hii ni Bid´ah. Haifai kwa mtu kufanya hivi. Anayetaka kunywa anahesabu wakati wake na wala hahitajii wewe umzindue.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://miraath.net/ar/content/fatawa/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%AF%D8%A7%D8%A1-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%83%D8%A8%D8%B1%D8%A7%D8%AA-%D8%A8%D9%82%D9%88%D9%84-%D8%A7%D8%B4%D8%B1%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%A7%D8%A1-%D9%82%D8%A8%D9%84-%D8%A3%D9%86-%D9%8A%D8%B7%D9%84%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D8%A8%D8%AD%D8%9F
  • Imechapishwa: 26/11/2017