“Wewe nimekutaliki ukitoka nyumbani” – imepita?


Swali: Kumetokea talaka kati ya wazazi wangu kutokana na sababu miongoni mwa sababu. Baba yangu alimwambia mama yangu: “Nimekutaliki ukitoka nyumbani.” Mama hakusikia ambapo akawa ametoka na hivyo talaka ikawa imetokea. Hii ilikuwa ni talaka ya tatu. Ni yepi maoni yako?

Jibu: Maoni yangu ni kwamba talaka haikupita.

Mosi ni kwa sababu mwanamke hakusikia. Hakukupitika uasi.

Pili ni kwamba mara nyingi wale wanaosema maneno kama haya hawakusudii kuwataliki wake zao, bali wanachokusudia ni kuwazuia kutoka. Tukikadiria kuwa ametoka kwa kukusudia basi analazimika kutoa kafara ya yamini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1052
  • Imechapishwa: 11/06/2019