Wewe na al-Hallaaj

Enyi waja wa Allaah! Tafakafirini ´Aqiydah ya al-Hallaaj. Yeye ndiye ambaye alikuwa kiongozi wa Qaraamitwah na walinganizi wa mazanadiki. Kuwa mwenye inswafu, jichunge na mche Allaah. Ifanyie hesabu nafsi yako. Ikikuthibitikia kuwa mtu huyu yuko na sifa zilizo na watu ambao ni maadui wa Uislamu, mwenye kupenda uongozi, mwenye kupenda umaarufu kwa hali zote, basi unatakiwa kujitenga mbali na ´Aqiydah yake.

Na ikikuthibitikia kuwa alikuwa amepatia na kwamba alikuwa ni mwongofu na mwenye kuongoza, basi unatakiwa kuufanya upya Uislamu wako na mwombe Mola wako akuwafikishe katika haki na akufanya imara juu ya dini yako. Kwani hakika uongofu  ni nuru ya Allaah ambayo Allaah huiweka ndani ya moyo wa mja Wake muislamu.

Ukiwa na  mashaka, usitambue uhakika wake na ukajitenga mbali na yale yote anayotuhumiwa, basi umeipumzisha nafsi yako na hivyo Allaah hatokuuliza juu yake.