Swali: Mwenye kusema kwamba sisi wasaudi, Wahhaabiyyuun na ni wenye ushabiki. Tumjibu vipi?

Jibu: Mwambie kwamba sisi Wahhaabiyyuun na waislamu. Lakini sio wenye ushabiki. Yeye ni mjinga. Ajifunze ndipo ataijua haki. Haki haitambuliki kupitia wanachuoni. Lakini wanachuoni wanatambulika kupitia haki, kuzisoma dalili na kuzizingatia. Chenye kuzingatiwa ni dalili. Wafuasi wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sio wenye kasumba na ushabiki. Wenye ushabiki ni wale wenye kufuata kichwa mchunga ambao wanawafuata watu wa batili katika upotofu wao kwa sababu tu eti ni waalimu zake, baba zake, babu zake au kwa sababu ni marafiki zake. Matokeo yake anawafuata na kuwafuata kibubusa. Huu ndio ushabiki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 44
  • Imechapishwa: 19/06/2019