Wenye kufuga ndevu wanafuga kwa kutii amri ya Mtume

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya mwenye kunyoa ndevu bali anamfanyia maskhara ambaye ameachia ndevu na anamuamrisha kuzinyoa?

Jibu: Haijuzu kufanya mzaha na mwenye kuachia ndevu zake. Ameziachia kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Linalotakiwa ni kumnasihi mwenye kufanya mzaha na kumwelekeza na kumbainishia kuwa kufanya kwake mzaha huku kumfanyia ambaye anafuga ndevu zake ni dhambi kubwa. Mwenye kufanya hivo kunachelea juu yake akaritadi kutoka katika Uislamu. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (09:65-66)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/35-36)
  • Imechapishwa: 24/08/2020