Wenye kuacha kufunga wanatakiwa kuadhibiwa na kutiwa adabu

Swali: Je, anakufuru yule anayeacha kufunga pasi na maradhi wala sababu nyingine lakini hata hivyo anaswali?

Jibu: Mwenye kuacha kufunga hali ya kupinga uwajibu wake anakufuru kwa maafikiano. Mwenye kuacha kwa sababu ya uvivu na uzembe hakufuru. Lakini hata hivyo yuko katika khatari kubwa kwa kuacha moja ya nguzo za Uislamu ambayo kuna maafikiano juu ya uwajibu wake. Mtu kama huyu anastahiki kuadhibiwa na kutiwa adabu na mtawala kwa mambo yatayomtia khofu yeye na watu mfano wake. Bali kuna wanachuoni wenye kuonelea kuwa ni kafiri. Ni wajibu kwake kulipa yale masiku aliyoyaacha na atubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/143)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Imechapishwa: 30/05/2017