Swali: Ni lipi bora kuwafanyia wazazi wawili; swadaqah au kuwaombea du´aa?
Jibu: Kuwafanyia yote mawili. Ikiwa hali zao za kifedha wanahitajia kusaidiwa, awape pesa na wakati huohuo asiwe bakhili wa du´aa. Akusanye kati ya kuwapa pesa na kuwaombea du´aa. Ama ikiwa ni matajiri, awaombee du´aa tu. Na akitaka kuwapa zawadi wote wawili au mmoja wao, hii ni kheri juu ya kheri.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (02)
- Imechapishwa: 06/09/2020