Wazazi wanataka mtoto arudi nyumbani na aache masomo


Swali: Mimi ni mwanafunzi ninayesoma katika chuo kikuu. Familia yangu wanataka niache kusoma katika chuo kikuu na nifanye kazi katika mji ambao wanaishi. Pamoja na kuwa mimi nikifanya kazi katika mji huo au mwingine basi nachelea moyo wangu kuwa mgumu kwa sababu nilijaribu kufanya hivo kabla ya kuanza chuo kikuu. Je, nikiendelea kusoma kwenye chuo kikuu hichi pamoja na hali ndio hii nitakuwa ni wenye kuwaasi wazazi?

Jibu: Huku sio kuwaasi wazazi. Ikiwa kuwa kwako mbali na wazazi na familia yako kunakuzidishia elimu yako na kunafanya imani yako kuwa na nguvu, basi endelea kufanya hivo. Huku sio kuwaasi wazazi. Unaweza kuwatembelea wazazi wako kwa mwezi mara moja au mara mbili kwa kiasi cha vile itavyokusahilikia. Vilevile jengine ni kwamba unaweza kuwapigia simu asubuhi na jioni kwa kutumia simu.

Ikiwa tutakadiria kuwa wazazi wanakuhitajia kilazima, basi katika hali hii tunasema kuwa ni lazima kutatua haja zao. Vinginevyo ikiwa hawana haja na wewe na wao wanachotaka tu ni uwe kwao na wewe unaona kuwa uwepo wako katika mji wanaoishi kunakuathiri, basi katika hali hii baki katika nchi ambayo inakuzidishia elimu na imani yako na wakati huohuo uwe ni mwenye kuwatendea wema wazazi kwa njia mbalimbali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/866
  • Imechapishwa: 01/07/2018