Wazazi wanakataza kuwasiliana na ndugu wengine

Swali: Tunakujuza kwamba tunakupenda kwa ajili ya Allaah. Umezungumzia juu ya kuwatendea wema wazazi wawili. Ikiwa wazazi hawa wawili hawaruhusu kuwatembelea ndugu muasi. Ni ipi hukumu ya kwenda kinyume nao katika jambo hilo?

Jibu: Swali hili ambalo ameuliza ndugu yetu hutokea mara nyingi. Wakati filani kunatokea kati ya mama na dada yake au ndugu zake wengine, kati ya baba na kaka yake au ndugu zake wengine kuelewana kimakosa. Wnaawaambia wanao kwamba wasimtembelee fulani kwa mfano shangazi yenu. Hapana shaka kwamba haya ni maamrisho ya kuwakata ndugu. Ni maamrisho ya maovu au mema? Ni maovu. Hivyo wawazi hawatakiwi kutiiwa katika jambo hili. Lakini mtu anatakiwa anatakiwa kuwafanyiwa ujanja; aende kuwatembelea kwa uficho wale aliokatazwa mtu asiwatembelee bila wazazi kujua jambo hilo. Hapo atakuwa amekusanya kati ya kufikia manufaa na kuzuia madhara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1336
  • Imechapishwa: 12/11/2019