Swali: Je, mama na baba yake na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni katika Ahl-ul-Fatrah?

Jibu: Enyi ndugu, sio katika Ahl-ul-Fatrah. Walikuwa na dini ya Ibraahiym. Walikuwa na dini ya Manabii ya watu waliopewa Kitabu. Sio katika Ahl-ul-Fatrah kwa kuwa walifikiwa na ulinganizi na ujumbe. Sio katika Ahl-ul-Fatrah. Ahl-ul-Fatrah ni wale ambao hawakufikiwa na kitu na hawakusikia hata kama kuna Mtume wala Kitabu. Walibaki kama walivyozaliwa na mama zao. Hawa ndio Ahl-ul-Fatrah.

Ama hawa wengine walifikiwa na ulinganizi wa Mitume. Isitoshe walibakiwa na mabaki [ya dini ya Ibraahiym]. Je, kabla ya kuja Uislamu watu hawakuwa wanaenda kuhiji? Walikuwa wanahiji, wakitufu, kufanya Say´ na kutoa Swadaqah. Haya ni katika mabaki ya dini ya Ibraahiym na Manabii. Walifikiwa na ulinganizi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020