Wazazi makafiri wanamzuia mtoto kwenda msikitini

Swali: Ni vipi muislamu atatangamana na wazazi wake makafiri ambao wanauchukia Uislamu na wanamkatalia kwenda msikitini kuswali?

Jibu: Asiwatii kuhusiana na kutoenda msikitini. Aende msikitini. Awaasi katika hilo:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Wakikufanyia juhudi kwamba unishirikishe na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Lakini suhubiana nao kwa wema duniani na fuata njia ya anayerudi Kwangu. Kisha Kwangu ndio marejeo yenu na nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.” (31:15)

Watendee wema. Lakini hata hivyo usiwatii katika maasi:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017