Swali 340: Akiwepo kijana anayetaka kutafuta elimu na wazazi wake wanamkataza na wanachotaka ni yeye aende katika Jihaad. Je, awatii katika jambo hilo?

Jibu: Apambane na wao. Haijuzu kwake kwenda ilihali wazazi wake wanamkataza. Kuhusu kujifunza elimu ambayo Allaah amemuwajibishia basi:

“Hakika hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kama ilivyo katika “al-Masaa-il” ya Ibn Haaniy (Rahimahu Allaah) ambaye amesimulia: “Kuna mtu alimuuliza Imaam Ahmad kuhusu mtu ambaye amekatazwa na baba yake, mama yake au wazazi wake kutafuta elimu akajibu:

“Asiwatii.”

Hilo ni tofauti na Jihaad. Vivyo hivyo iwapo mama yake atamkataza swalah ya mkusanyiko asimtii. al-Hasan al-Baswriy (Rahimahu Allaah) alisema hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 582
  • Imechapishwa: 07/12/2019