Swali: Je, waumini watatofautiana katika kumuona Allaah (´Azza wa Jall) Peponi?

Jibu: Ndio, kutegemea na matendo. Kunatofautiana kwa kutegemea matendo yao. Kumuona Allaah ni neema. Na neema zinatofautiana kama tulivyotangulia kusema. Peponi kuna daraja mbalimbali – tunamuomba Allaah tuwe miongoni mwao. Kila daraja ilivyo juu ndivo ina neema kubwa zaidi kuliko daraja ilio chini yake. Moto pia una daraja mbalimbali. Kila ambavo daraja ilivyo chini zaidi ndivo ina adhabu kali zaidi kuliko daraja ilo juu yake. Waumini wanatofautiana katika neema na katika kumuona Allaah. Miongoni mwao wako ambao watamuona asubuhi na jioni.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/16/%D8%A7%D8%AE%D8%AA%D9%84%D8%A7%D9%81-%D8%B1%D8%A4%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%A4%D9%85%D9%86%D9%8A%D9%86-%D9%84%D8%B1%D8%A8%D9%87%D9%85-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%86%D8%A9-%D8%A8%D8%AD%D8%B3%D8%A8-%D8%A3%D8%B9%D9%85%D8%A7%D9%84%D9%87%D9%85
  • Imechapishwa: 24/01/2020