Waumini na watawala


Swali: Unasemaje kwa yule mwenye kuwatukana watawala kwa sababu ya uhuru wa demokrasia?

Jibu: Madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kutofanya uasi kwa mtawala. Uasi unaweza kuwa kwa maneno, kutweza au kuwatusi, na kubebea silaha dhidi yao. Yote hayo ni kuwafanyia uasi watawala. Badala yake mtu anatakiwa kuwa na subira juu ya haki, kusaidiana katika wema na uchaji Allaah, kusubiria nyakati bora na kutokatika moyo. Hii ndio njia ya waumini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.miraath.net/ar/content/%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AD%D8%A7%D8%B6%D8%B1%D8%A7%D8%AA/%D9%88%D8%B5%D8%A7%D9%8A%D8%A7-%D9%85%D9%87%D9%85%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%B2%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%81%D8%AA%D9%86
  • Imechapishwa: 16/09/2017