Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao: wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanasimamisha swalah na wanatoa zakaah na wanamtii Allaah na Mtume Wake – hao Allaah atawarehemu. Kwani hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa, Mwenye hekima.”[1]

Amefanya katika sifa zao ni kwamba wanaamrisha mema na wanakataza maovu. Ambaye haamrishi mema na hakatazi maovu ni miongoni mwa wanafiki. Amesema (Ta´ala):

الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُم مِّن بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ

“Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake wenyewe kwa wenyewe: wanaamrisha maovu na wanakataza mema.”[2]

Wao wako kinyume. Hivi sasa hapa wanaamrisha maovu. Bali wanaamrisha maovu kwa aina zake zote, wanalingania kwayo, wanawalingania waislamu kuiacha dini yao, wanaita kushikamana barabara na dini kwamba ni msimamo mkali na uchupaji mpaka. Wanasema kwamba ni lazima waislamu waachane na jambo hilo. Wanasema kwamba ni lazima kwa wanawake wafanye uasi wa kindoa na waachane na Hijaab, kwamba watu waache kuwapenda waumini peke yake na kuwachukia makafiri na kwamba wawafanye watu wote kuwa sawasawa na wasiwatofautishe. Huku ni kuamrisha maovu. Wao wanaamrisha maovu na wanakataza maovu siku zote na daima. Kinyume cha waumini ambao wanaamrisha mema na kukataza maovu.

Kuamrishana mema na kukatazana maovu ni miongoni mwa mambo ya lazima ya dini. Ni jambo ambalo ni la lazima katika Uislamu. Kukipatikana jambo la kuamrishana mema na kukatazana maovu basi hiyo ni alama ya kufaulu kwa Ummah. Kukikosekana jambo la kuamrishana mema na kukatazana maovu basi hiyo ni alama ya kuangamia kwa Ummah.

[1] 09:71

[2] 09:67

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydatu al-Imaam-il-Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 139
  • Imechapishwa: 02/02/2020