Waume bora hawawapigi wake zao 


Abu Daawuud amesema:

2146 – Ahmad bin Abiy Khalaf na Ahmad bin ‘Amr bin as-Sarh ametueleza: Sufyaan ametueleza, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘AbdillaaH:  Ibn-us-Sarh ‘Ubaydullaah bin ‘Abdillaah ametueleza kutoka kwa Iyaas bin ‘Abdillaah bin Abiy Dhubaab ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwapige wajakazi wa Allaah.” Akaja ´Umar na kusema: “Wanawake wanawaasi waume zao.” Hivyo akaacha wanawake wawe wanapigwa. Wakaja wanawake wengi kwa wakeze Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwashtaki waume zao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wanawake wengi wamekuja kwa wakeze Muhammad na wanawashtaki waume zao. Hao sio katika wabora wenu.”[1]

Hadiyth hii inatolea dalili kwamba inajuzu kumpiga mke ikiwa hatekelezi majukumu ya ndoa. Hata hivyo kipigo hakitakiwi kuwa cha kuumiza. Hadiyth inatolea dalili vilevile kwamba ni bora kuwa na subira juu ya tabia yao mbaya na mienendo yao ya utovu wa adabu.

[1] Imaam al-Albaaniy amesema:

“Hadiyth inatiliwa nguvu na Hadiyth hizi zingine mbili kwa hiyo inakuwa nzuri (Hasan).” (Ghaayat-ul-Maraam, uk. 156)

  • Mhusika: Imaam Abu Sulaymaan Hamad bin Muhammad al-Khattwabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma-aalim-us-Sunan (3/220-221)
  • Imechapishwa: 20/09/2020