Wauguzi wa kike ni Malaika wa rehema?

Swali: Mara nyingi tunasoma na kusikia kutoka kwa watu wa kawaida kupitia maandishi na mashairi yao wanaoeleza kuwa wauguzi wa kike ni Malaika wa rehema. Unasemaje juu ya wasifu kama huu?

Jibu: Haijuzu kutumia wasifu huu juu ya wauguzi wa kike. Malaika ni waume na si wake. Allaah (Subhaanah) amewakemea washirikina kuwasifu Malaika uke. Isitoshe Malaika wa rehema wanazo sifa maalum wasizokuwa nazo wauguzi wa kike. Jengine wauguzi wa kike miongoni mwao wako wazuri na wabaya. Kwa hivyo haijuzu kutumia wasifu huu juu yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/423)
  • Imechapishwa: 02/07/2021