Fuateni mfumo wa Salaf! Tazameni wanachuoni wamezalisha wanaume wangapi wenye elimu na uelewa. Kama mfano wa Shaykh Ibn Baaz, Shaykh Ibn ´Uthaymiyn, Shaykh Muqbil, Shaykh al-Albaaniy, Shaykh al-Fawzaan na wanachuoni wengineo. Tazameni namna ambavyo wamewafunza watu Qur-aan na Sunnah na kutunga vitabu vyenye faida na vya thamani. Allaah amewanufaisha watu kwa elimu yao na ulinganizi wao mpaka hii leo. Miongoni mwao kuna ambao wameshakufa na wengine bado wako hai, lakini bado mpaka hii leo faida zinaendelea. Lau watu wote wangelikuwa na mfumo kama wa Usaamah bin Laadin ingelikuwa ni msiba mkubwa. Wanachuoni wote wangelikuwa na mfumo kama wa Usaamah bin Laadin, Sayyid Qutwub, Muhammad Suruur na Muhammad Qutwub moto ungeliwaka. Miji ya Kiislamu ingelikuwa inawaka moto. Watu walioko ni wenye busara, wenye dini, wanachuoni na wasomi wenye uelewa na Allaah amenufaisha kwa elimu yao na kwa ulinganizi wao. Upande wa pili watu hawa moto ndio ungeliwaka. Mfumo wa Usaamah bin Laadin, Muhammad Qutwub, Sayyid Qutwub, Hasan al-Banna na Muhammad Suruur imeleta madhara makubwa mno katika jamii za Kiislamu. Madhara yake yanaendelea mpaka hii leo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ath-Thabaat ´alaa as-Swiraat al-Mustaqiym yakuun bil-´Ilm http://olamayemen.com/Dars-9998
  • Imechapishwa: 04/05/2018