572- Baba yangu aliulizwa kuhusu watu wenye kuchelewa swalah ya ijumaa. Akajibu:

”Ibn Mas´uud aliswali na ´Alqamah na al-Aswad.”

Bi maana aliswali nao swalah ya ijumaa.

573- Siku moja nilichelewa swalah ya ijumaa na hivyo tukaiswali kwa pamoja msikitini. Baada ya hapo nikamweleza hilo baba yangu ambapo akatabasamu na hakunikemea.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (2/406)
  • Imechapishwa: 29/01/2021