Watu wawili wanaweza kushirikiana katika kondoo au mbuzi katika Udhhiyah?


Swali: Inajuzu kwa mwenye uwezo kuchinja zaidi ya Udhhiyah mmoja kwa vile imepokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja mbuzi/kondoo wawili? Je, mume na mke wanaweza kushirikiana katika mbuzi/kondoo mmoja ambapo kila mmoja anatoa thamani ya nusu yake? Yupi kati ya hawa anayetakiwa kujizuia?

Jibu: Bora ni mtu kutozidisha juu ya mbuzi/kondoo mmoja kwake yeye na familia yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja mbuzi/kondoo mmoja juu yake yeye na familia yake. Ni jambo linalojulikana ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mkarimu zaidi na kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye kiumbe anayependa kumuabudu Allaah na kumuadhimisha.

Kuhusu kwamba alichinja mbuzi/kondoo wawili wote wawili hawakuwa kwa ajili yake na familia yake. Yule wa pili alikuwa kwa ajili ya Ummah wake. Kujengea juu ya haya bora ni kukomeka juu ya mbuzi/kondoo mmoja juu ya baba mwenye nyumba na familia yake. Yule aliye na pesa zaidi basi awape hizo, chakula au kitu kingine nchi zengine zinazohitajia au wahitaji katika nchi yetu. Nchi yetu pia haikosi watu wenye kuhitaji.

Kuhusu mume na mke kushirikiana katika mbuzi/kondoo mmoja ni jambo lisilosihi. Haifai watu wawili wakashirikiana juu ya kile kima katika mbuzi/kondoo mmoja. Ushirikiano zaidi ya mtu mmoja unakuwa katika ngamia na ng´ombe. Ngamia inakuwa watu saba. Ng´ombe pia inakuwa watu saba. Ama kuhusu  mbuzi na kondoo haiwezekani kamwe kwa watu wawili wakashirikiana. Thawabu hazina kikomo. Hakuna ubaya ukaomba kwa kusema:

“Ee Allaah! Hii ni kwa ajili yangu mimi na mke wangu.”

“Ee Allaah! Hii ni kwa ajili yangu mimi na familia yangu.”

Ama kusema kila mmoja atoe nusu ya thamani yake na wakanunua kondoo au mbuzi mmoja kwa ajili ya Udhhiyah si sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/752
  • Imechapishwa: 10/08/2019