Swali: Wale wanaotukana wanachuoni wetu na kuwaita kwamba ni wasomi wa hedhi[1] na nifasi na wanasema kwamba tusifarikishe kati ya vijana wa Ummah na kwamba eti wanataka umoja. Je, huku ni kukufuru yale aliyoteremsha Allaah na Mtume wake?

Jibu: Hii sio kufuru. Lakini huku ni kusengenya na ni kuvunja heshima ya wanachuoni. Kitendo hichi ni haramu pasi na shaka. Kusengenya kumeharamishwa vibaya sana. Ni wajibu kwao kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Isitoshe kuna faida gani ya kuwasema vibaya wanachuoni? Hakuna faida yoyote isipokuwa shari tupu. Anawafanya watu kuwachukia na kuwafanya uaminifu kwao unakuwa mchache.  Watu wasiporejea kwa wanachuoni watarejea wapi? Wataenda wapi? Ni khatari kubwa.

[1] Tazama https://www.youtube.com/watch?v=toPN9LCFwi4

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 126
  • Imechapishwa: 30/11/2018