Hatutakiwi kufahamu Qur-aan na Sunnah kwa mujibu wa fahamu zetu fupi. Viwili hivyo vinatakiwa kufahamika kwa mujibu wa as-Salaaf as-Swaalih:

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا

“Basi wakiamini kama vile mlivyoyaamini nyinyi, basi kwa hakika watakuwa wameongoka.” (02:137)

Bi maana Qur-aan na Sunnah kwa uelewa wa Maswahabah:

وَّإِن تَوَلَّوْا

“… na wakikengeuka… “

Bi maana wanafuata Qur-aan na Sunnah lakini sio kwa ufahamu wa Maswahabah, bali kwa ufahamu wa Sayyid Qutwub, Muhammad Qutwub, Hasan al-Bannaa, Muhammad Suruur na wapotevu wengine waliokuja nyuma. Wakikataa kuwa na uelewa kama waliokuja nao Maswahabah:

وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ

“… na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani… “

Wanafanya mipasuko, wanatawanyisha, wanasababisha fitina, wanaleta matatizo, wanaua, vita, wanaandamana, wanachokoza, wanafunga umeme na maji, wanavunja mimea na majanga chungunzima:

وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

“… na wakikengeuka basi hakika wao wamo katika upinzani, basi Allaah Atakutosheleza nao – Naye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.” (02:137)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://olamayemen.al3ilm.com/
  • Imechapishwa: 22/05/2022