Swali: Kipindi cha mwisho imeenea kwa baadhi ya wenye dini watu wanaopunguza ndevu zao. Ni mpaka upi unaojuzu kupunguza ndevu pamoja na kujua ya kwamba wakati tunapowanasihi juu ya mambo kama hayo wanasema “haya ni masuala ya tofauti”?

Jibu: Kitu ambacho kimefanya kuchinjana na kupigana vita ni msemo wao “Haya ni masuala wametofautiana”. Ndugu! Allaah hakufanya tukaabudu kwa tofauti. Allaah Amefanya kuabudu kwa dalili kutoka kwenye Qur-aan na Sunnah. Ni kweli wanachuoni wanatofautiana. Lakini lililo la wajibu juu yetu ni kuchukua yale yaliyosimama juu ya dalili:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho.” (04:59)

La sivyo tutakuwa kama mayahudi na manaswara:

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ

“Wamewafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allaah.” (09:31)

bi maana yale wanayohalalisha na sisi tunahalalisha, wanayoharamisha na sisi tunaharamisha na tunasema “Masuala haya yana tofauti”. Huu ni upotevu na tunaomba kinga kwa Allaah. Hakuna anayesema hivi isipokuwa mtu ambaye ima ni mjinga au mkaidi ambaye ndani ya moyo wake hamna Imani[1].

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuna-tofauti-katika-mambo-haya-ima-mjinga-au-jitu-linalofuata-matamanio/.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-03-17.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014