Swali: Ni ipi hukumu kwa mtu kuitwa kwa Majina ya Allaah kama kumwita mtu al-´Aziyz? Silichukulii hilo kama sifa yake bali kama jina tu.

Jibu: Majina ya Allaah yako aina mbili:

1- Aina ambayo ni maalum Kwake tu. Haijuzu kwa yeyote kujiita kwayo. Kama mfano wa Allaah, ar-Rahmaan, al-Jabbaar na al-Mutakabbir. Majina kama haya haijuzu kwa yeyote katika viumbe kujiita kwayo.

2- Aina ya pili sio maalum kwa Allaah na inajuzu kwa asiyekuwa Yeye kujiita kwayo. Hapa ni pale ambapo mtu hakusudii kuwa jina hili [alilomwita kwalo] linatolea dalili maana yake. Mfano wa hili ni kama kumwita mtu ´Aziyz na kuamini kwamba mtu huyu ana ukuu na utukufu. Hili halijuzu. Ama ikiwa inakusudiwa kuwa ni jina tu na hakukusudiwi ndani yake kitu katika maana, hili halina neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (11 A)
  • Imechapishwa: 06/10/2020